Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023Mfano
Hata baada ya Mungu kuonyesha uweza wake, Waisraeli bado walitafuta na kuabudu miungu, na Mungu wa kweli akaudhika. Kwa hiyo Mungu alihukumu Efraimu, kabila kiongozi, na kuondoa hema ya kukutania iliyokuwa katika nchi yake:Hakuichagua kabila la Efraimu(m.67) ...akaiacha maskani ya Shilo, Hema aliyoiweka katikati ya wanadamu(m.60). Lakini uaminifu wa Mungu haubadiliki. Kwa hiyo akawainulia watu wake mtawala mwingine, mfalme Daudi, ambaye aliwaongoza kwa haki na uadilifu, akawa mfano wa Kristo Yesu:Akawalisha kwa ukamilifu wa moyo wake, Na kuwaongoza kwa busara ya mikono yake(m.72). Habari hiyo itutie moyo kumrudia Mungu na kumtegemea. Mungu anaaminika!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Oktoba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Yohana na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/