Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 78:56-72

Zab 78:56-72 SUV

Lakini walimjaribu Mungu Aliye juu, wakamwasi, Wala hawakuzishika shuhuda zake. Bali walirudi nyuma, wakahaini kama baba zao; Wakaepea kama upinde usiofaa. Wakamkasirisha kwa mahali pao pa juu, Wakamtia wivu kwa sanamu zao. Mungu akasikia, akaghadhibika, Akamkataa Israeli kabisa. Akaiacha maskani ya Shilo, Hema aliyoiweka katikati ya wanadamu; Akaziacha nguvu zake kutekwa, Na fahari yake mkononi mwa mtesi. Akawatoa watu wake wapigwe kwa upanga; Akaughadhibikia urithi wake. Moto ukawala vijana wao, Wanawali wao hawakuimbiwa nyimbo za arusi, Makuhani wao walianguka kwa upanga, Wala wajane wao hawakuomboleza. Ndipo Bwana alipoamka kama aliyelala usingizi, Kama shujaa apigaye kelele sababu ya mvinyo; Akawapiga watesi wake akawarudisha nyuma, Akawatia aibu ya milele. Ila akaikataa hema ya Yusufu; Wala hakuichagua kabila ya Efraimu. Bali aliichagua kabila ya Yuda, Mlima Sayuni alioupenda. Akajenga patakatifu pake kama vilele, Kama dunia aliyoiweka imara milele. Akamchagua Daudi, mtumishi wake, Akamwondoa katika mazizi ya kondoo. Nyuma ya kondoo wanyonyeshao alimwondoa, Awachunge Yakobo watu wake, na Israeli urithi wake. Akawalisha kwa ukamilifu wa moyo wake, Na kuwaongoza kwa busara ya mikono yake.