Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023

SIKU 8 YA 31

Baada ya kusoma mistari 18 ya kwanza ya sura hii, mambo mawili yapo wazi:1.Kaburi ni tupu! Mwili wa Yesu haumo. Ndiyo alivyoona yule mwanafunzi:Akainama na kuchungulia, akaona vitambaa vya sanda vimelala; lakini hakuingia. Basi akaja na Simoni Petro, akaingia ndani ya kaburi; akavitazama vitambaa vilivyolala, na ile leso iliyokuwako kichwani pake; haikulala pamoja na vitambaa, bali imezongwa-zongwa mbali mahali pa peke yake(m.5-7)!2.Sababu ya kaburi kuwa tupu ni kwamba Yesu yu hai, amefufuka. Yohana anaandika:Basi ndipo alipoingia naye yule mwanafunzi mwingine aliyekuwa wa kwanza wa kufika kaburini, akaona na kuamini. Kwa maana hawajalifahamu bado andiko, ya kwamba imempasa kufufuka(m.8-9)! Kwa kumfufua Yesu, Mungu amethibitisha kuwa yeye ndiye Mwana wa Mungu, na Mungu ameipokea kazi yake ya upatanisho! Kwa njia hii Yesu alipata uwezo mkuu:Wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyikawatoto wa Mungu(Yn 1:12).Ninapaa kwenda kwa Baba yangunaye ni Baba yenu(m.17)!

siku 7siku 9

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Oktoba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Yohana na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana