Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023

SIKU 7 YA 31

Ni siku ya tatu tangu Yesu alipowekwa kaburini. Alikufa Ijumaa. Jumamosi ikawa sabato ya Pasaka (19:31,Basi Wayahudi, kwa sababu ni Maandalio, miili isikae juu ya misalaba siku ya sabato, (maana sabato ile ilikuwa siku kubwa), walimwomba Pilato miguu yao ivunjwe, wakaondolewe). Na sasa ni Jumapili,siku ya kwanza ya juma(m.1). Mariamu alipoona kwamba jiwe limeondolewa akaenda haraka kutoa habari kwaSimoni Petro na kwa yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, akawaambia, Wamemwondoa Bwana kaburini, wala hatujui walikomweka(m.2). Yohana hataji jina lake mwenyewe, maana yeye ndiye mwandishi wa Injili hii. Mariamu hasemi "sijui" bali"hatujui walikomweka” (m.2),maana alikuwa pamoja na wanawake wengine (Mk 16:1-4).

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Oktoba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Yohana na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana