Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023

SIKU 6 YA 31

Kabla Yesu hajafa alisema,Imekwisha(m.30). Kwa tafsiri nyingine alisema,Yametimia. Imekwisha nini? Kazi yake ya wokovu imekwisha:Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ... Hakuna aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe ... Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu(Yn 10:17-18). Kitu gani kimetimia? Yametimia Maandiko yasemayo kwamba ndivyo alivyotakiwa Masihi kuteseka kwanza kabla hajatukuzwa na kupewa mamlaka yote Mbinguni na duniani.Hayo yalitukia ili andiko litimie, Hapana mfupa wake utakaovunjwa. Na tena andiko lingine lanena, Watamtazama yeye waliyemchoma(36-37). Yesu mwenyewe pia alionyesha Maandiko yanavyomshuhudia,Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia(Yn 5:39).

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Oktoba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Yohana na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana