Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023

SIKU 5 YA 31

Kwenye msalaba juu ya kichwa cha Yesu paliandikwa:YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI. Ni maneno ya kweli! Utukufu wa Yesu si nguo, maana nguo zake walizichukua,wakafanya mafungu manne, kwa kila askari fungu lake; na kanzu nayo. Basi kanzu ile haikushonwa, ilikuwa imefumwa yote pia tangu juu. Basi wakaambiana, Tusiipasue, lakini tuipigie kura, iwe ya nani. Ili litimie andiko lile linenalo, Waligawanya nguo zangu, Na vazi langu wakalipigia kura. Basi ndivyo walivyofanya wale askari(m.23-24). Utukufu wake ni taji ya miiba na damu (19:1-5,Askari wakasokota taji ya miiba, wakamtia kichwani, wakamvika vazi la zambarau. Wakawa wakimwendea, wakisema, Salamu! Mfalme wa Wayahudi! ... Ndipo Yesu alipotoka nje, naye amevaa ile taji ya miiba, na lile vazi la zambarau, Pilato akawaambia, Tazama, mtu huyu!). Je, hayo kweli ni utukufu? Ndiyo! Maana Yesu alikubali hayo yote kwa hiari, na kwa upendo mkuu. Wanadamu ndio tumestahili hukumu kama hii kwa sababu ya dhambi zetu! LakiniYesu alikufa badala yetu!Je, umemtukuza Yesu kwa hayo? Unaweza kutumia sifa hizi kumtukuza:Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi(Ufu 5:9-10).

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Oktoba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Yohana na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana