Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 01/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 01/2024

SIKU 15 YA 31

Amri ya sita inasema, Usizini. Yesu anatoa mkazo juu ya amri hii kwamba isitazamwe katika hali ya nje tu, maana uovu huanzia ndani ya moyo wa mtu. Wakati wa Musa kulikuwa na tatizo la maisha ya ndoa. Hali hiyo ikapelekea kuruhusu mume kumpa talaka mke. Biblia inasema Musa alifanya hivi kwa sababu ya ugumu wa mioyo ya watu. Huo haukuwa mpango wa Mungu. Katika Mk 10:6-12 tunapata mafundisho ya ndoa ya Kikristo kwa mpango wa Mungu. Yesu anaeleza,Tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke.Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.Hata nyumbani tena wanafunzi wakamwuliza habari ya neno hilo.Akawaambia, Kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake;na mke, akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine, azini.Tafakari maana yake kwako kwamba sisi Wakristo tunapaswa kuishi kulingana na Neno la Mungu.

siku 14siku 16

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2024

Soma Biblia Kila Siku 01/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/