Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 01/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 01/2024

SIKU 19 YA 31

Inatakiwa tuifanye kazi ya Mungu bila kuwa na unafiki wowote. Yesu anataka tujue kwamba, tunapofunga na kuomba, silo jambo la kujionyesha kwa wengine kwamba sisi ni wacha Mungu. Mungu anaangalia mioyo yetu. Tunachofanya sirini si siri kwake. Kuwa Mkristo wa kweli ni ile hali ya mtu kujitambua kwamba yeye mwenyewe hawezi lolote ila anamhitaji Mungu aliye Mtakatifu. Zingatia namna tunavyotakiwa kuwa na nia na mawazo yanayotuelekeza kwa Mungu anayetuwazia yaliyo mema, kwa kusoma Yn 4:19-24:Yule mwanamke akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u nabii!Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia.Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu.Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi.Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.

siku 18siku 20

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2024

Soma Biblia Kila Siku 01/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/