Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 01/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 01/2024

SIKU 23 YA 31

Katika safari ya kwenda mbinguni, mwanadamu yeyote anakabiliwa na mtihani wa kuchagua mojawapo kati ya njia mbili. Njia pana ambayo wengi huipenda, inaonekana ni rahisi kuiendea, lakini mwisho wake ni upotevuni. Walimu wake huonekana kama kondoo, lakini kumbe ni hatari kama mbwa mwitu. Na njia ya pili ni nyembamba na ya kujikana kwa ajili ya Bwana Yesu. Ndiyo inayowapeleka watu kwenye uzima wa milele. Wanaosikia sauti ya Yesu na kuitii, hupita njia hii. Je, wewe umechagua njia ipi?

siku 22siku 24

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2024

Soma Biblia Kila Siku 01/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/