Soma Biblia Kila Siku 01/2024Mfano
Mistari hii ni mwendelezo wa masikitiko ya Daudi dhidi ya maadui zake. Daudi anasikitika zaidi anapoona kuwa washambuliaji wake ni wale aliowasaidia, aliopendana nao, na kuwaombea walipokuwa katika shida (m.11-14,Mashahidi wa udhalimu wanasimama, Wananiuliza mambo nisiyoyajua. Wananilipa mabaya badala ya mema, Hata nafsi yangu ikaingia ukiwa.Bali mimi, walipougua wao, Nguo yangu ilikuwa gunia. Nalijitesa nafsi yangu kwa kufunga; Maombi yangu yakarejea kifuani mwangu.Nalijifanya kama kwamba ni rafiki au ndugu yangu, Naliinama nikilia kama aliyefiwa na mamaye). Maadui hao wanashabikia na kutaka Daudi akamatwe haraka ili waweze kumwangamiza. Kama katika mistari iliyotangulia, Daudi anamtegemea Mungu kwani anajua kwamba Mungu pekee anaweza kumhifadhi na kumtia nguvu asishindwe na mashamulio hayo (m.15-18, Nikijikwaa hufurahi na kukusanyana, Walinikusanyikia watu ovyo nisiowajua, Wananipapura wala hawakomi.Kama wenye mzaha wakikufuru karamuni Wananisagia meno.Bwana, hata lini utatazama? Uiokoe nafsi yangu na maharabu yao, Na mpenzi wangu na wana-simba.Nitakushukuru katika kusanyiko kubwa; Nitakusifu kati ya watu wengi).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 01/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/