Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 01/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 01/2024

SIKU 30 YA 31

Kila mmoja wetu ameonja namna fulani ya ugumu katika maisha. Kama wewe ni mmojawapo, je, unafanyaje ili kushinda hali hii? Mfalme Daudi alitambua kwamba Mungu ndiye kimbilio lake, kwani hakuna wa kufanana naye. Nasi tupatwapo na matatizo tujiangalie tusije tukategemea njia za uovu au miungu mingine.Heri aliyemfanya Bwana kuwa tumaini lake, Wala hakuwaelekea wenye kiburi, Wala hao wanaogeukia uongo(m.4). Tumwambie Mungu, na tumngoje kwa saburi, naye atasikia kilio chetu. Atatupandisha toka shimo la uharibifu na kuisimamisha miguu yetu mwambani, kama Daudi anavyoshuhudia katika m.1-2,Nalimngoja Bwana kwa saburi, Akaniinamia akakisikia kilio changu.Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

siku 29siku 31

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2024

Soma Biblia Kila Siku 01/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/