Soma Biblia Kila Siku 01/2024Mfano
Maisha ya mwanadamu ni mafupi sana hapa duniani, na yamejaa shida nyingi. Hivyo hakuna sababu ya kujulimbikizia mali katika mji huu usiodumu. Daudi anajiona kama msafiri na kama mgeni apitaye. Anaona ni vema kukabidhi maisha yake kwa Mungu, ili Mungu amtendee mema katika siku chache za kuishi kwake hapa duniani (m.12-13,Ee Bwana, usikie maombi yangu, Utege sikio lako niliapo, Usiyanyamalie machozi yangu. Kwa maana mimi ni mgeni wako, Msafiri kama baba zangu wote.Uniachilie nikunjuke uso, Kabla sijaondoka nisiwepo tena). Tunakumbushwa kuwa vitu vya hapa ni vya kitambo kifupi ila vya mbinguni vinadumu miliele. Tunapaswa kuvichuchumilia vya mbinguni kama Mtume Paulo anvyoshauri,Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu(Kol 3:2-3).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 01/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/