Zab 39:7-13
Zab 39:7-13 SUV
Na sasa ninangoja nini, Ee Bwana? Matumaini yangu ni kwako. Uniokoe na maasi yangu yote, Usinifanye laumu ya mpumbavu. Nimenyamaza, sitafumbua kinywa changu, Maana Wewe ndiwe uliyeyafanya. Uniondolee pigo lako; Kwa uadui wa mkono wako nimeangamia. Ukimrudi mtu kwa kumkemea kwa uovu wake, Watowesha uzuri wake kama nondo. Kila mwanadamu ni ubatili. Ee BWANA, usikie maombi yangu, Utege sikio lako niliapo, Usiyanyamalie machozi yangu. Kwa maana mimi ni mgeni wako, Msafiri kama baba zangu wote. Uniachilie nikunjuke uso, Kabla sijaondoka nisiwepo tena.