Zaburi 39:7-13
Zaburi 39:7-13 SRUV
Na sasa ninangoja nini, Ee Bwana? Matumaini yangu ni kwako. Uniokoe kutoka kwa maasi yangu yote, Usinifanye niwe wa kulaumiwa na mpumbavu. Nimenyamaza, sifumbui kinywa changu, Maana Wewe ndiwe uliyeyafanya. Uniondolee pigo lako; Kwa mapigo ya mkono wako nimeangamia. Ukimrudi mtu kwa kumkemea kwa uovu wake, Watowesha uzuri wake kama nondo. Kila mwanadamu ni ubatili. Ee BWANA, usikie maombi yangu, Utege sikio lako niliapo, Usiyapuuze machozi yangu. Kwa maana mimi ni mgeni wako, Msafiri kama baba zangu wote. Uache kunitazama, ndio nipate kufurahi tena, Kabla sijafa na kutoweka kabisa.