Zaburi 39:7-13
Zaburi 39:7-13 BHN
Na sasa, ee Bwana, ninatazamia nini? Tumaini langu ni kwako wewe! Uniokoe katika makosa yangu yote; usikubali wapumbavu wanidhihaki. Niko kama bubu, sisemi kitu, kwani wewe ndiwe uliyetenda hayo. Usiniadhibu tena; namalizika kwa mapigo yako. Unapomwadhibu mtu dhambi zake kwa kumkemea, unaharibu kama nondo kile akipendacho. Hakika, kila binadamu ni kama pumzi tu! Usikie sala yangu, ee Mwenyezi-Mungu; usikilize kilio changu, usikae kimya ninapolia. Maana, mimi ni kama mgeni tu apitaye, ni msafiri kama walivyokuwa wazee wangu wote. Uache kunitazama nipate kufurahi kidogo, kabla sijaaga dunia, na kutoweka kabisa.