Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 39:7-13

Zaburi 39:7-13 NEN

“Lakini sasa Bwana, nitafute nini? Tumaini langu ni kwako. Niokoe kutoka kwenye makosa yangu yote, usinifanye kuwa dhihaka ya wapumbavu. Nilinyamaza kimya, sikufumbua kinywa changu, kwa sababu wewe ndiwe uliyetenda hili. Niondolee mjeledi wako, nimeshindwa kwa mapigo ya mkono wako. Unakemea na kuadhibu wanadamu kwa ajili ya dhambi zao; unaharibu utajiri wao kama nondo aharibuvyo: kila mwanadamu ni kama pumzi tu. “Ee BWANA, usikie maombi yangu, usikie kilio changu unisaidie, usiwe kiziwi kwa kulia kwangu. Kwani mimi ninaishi na wewe kama mgeni, kama walivyokuwa baba zangu wote, Tazama mbali nami, ili niweze kufurahi tena kabla sijaondoka na nisiwepo tena.”