Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 01/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 01/2024

SIKU 22 YA 31

Mungu hujibu maombi. Hufahamu haja zetu hata kabla hatujaomba. Ndiyo maana hutujalia kuyapata hata yale ambayo hatujayaomba.Mungu hutujalia kupata yaliyo mema kutoka kwake, wala hawezi kupuuzia tuliyoyaomba kwa jina lake. Sisi wanadamu tulio waovu huwa tunawapa watoto wetu zawadi nzuri. Hakuna mzazi anayeweza kumpa mwanawe nyoka badala ya samaki au jiwe badala ya mkate. Ni hakika kabisa, Mungu aliye Mtakatifu na Mwenye wema wote hutujalia kupokea mema zaidi ya yale tunayoomba.

Andiko

siku 21siku 23

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2024

Soma Biblia Kila Siku 01/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/