Soma Biblia Kila Siku 01/2024Mfano
Hali yetu ya kibinadamu inatufanya kuyaona makosa au udhaifu wa wengine kuliko wa kwetu. Hata tunakuwa wepesi wa kulaumu na kuwahukumu wengine. Neno la Mungu linatuonya kwamba anayeweza kuona na kutoa hukumu ya kweli ni Mungu tu, siyo mwanadamu. Na hapo ni lazima tujue kuwa maovu ya kila mtu yapo wazi mbele za Mungu. Vilevile tufahamu kuwa Yesu anajua kuwa kuna wale wanaoliheshimu Neno la Mungu katika hali ya ukweli, na kuna wale wanaolidharau na kulitumia kwa malengo yao wenyewe. Kuhusu hao Yesu anasema,Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua(m.6).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 01/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/