Soma Biblia Kila Siku 01/2024Mfano
Yohana Mbatizaji alihubiri akitii kwa unabii wa Isaya usemao:Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana(ling. Yn 1:23). Yohana aliwaandaa watu kumpokea mkombozi wao Yesu, aliyezaliwa. Wote walioungama dhambi zao aliwabatiza katika mto Yordani, akawaonya wazae matunda yapasayo toba. Wasijivune kuwa wamezaliwa kuwa watu wa Mungu, maana "Mungu aweza kuinua mawe yakawa watoto." Yaani sisi wa Mataifa twaweza kuwa wana wa Mungu, ila tusipozaa matunda ya toba hatutaepuka hukumu yake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 01/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/