Soma Biblia Kila Siku 01/2024Mfano
Epifania ni sikukuu ya kufunuliwa kwa Kristo Yesu. Wokovu wa Mungu unatangazwa kwa njia ya mfano wa nuru. Wokovu huu utaleta mabadiliko makubwa Yerusalemu na hata kwa mataifa yaliyo kinyume na Israeli. Waisraeli walioko utumwani wataachwa huru na kurudi Yerusalemu. Mataifa waliokuwa gizani watavutwa na nuru ya utukufu wa Mungu ulio na watu wake. Matukio hayo makubwa ni baada ya watu wa Mungu kuacha maasi na kumpokea Mkombozi (Isa 59:20,Mkombozi atakuja Sayuni, kwao waachao maasi yao katika Yakobo, asema Bwana). Nasi ambao tumepokea ukombozi kwa Yesu Kristo tunatumwa kuwa nura ya ulimwengu ili wote wamjie Yesu waokolewe.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 01/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/