Soma Biblia Kila Siku 02/2024Mfano
Ziko sheria zinazohusu kumkosesha mtu; nazile ambazo mtu anamkosea mwenzake. Kumkosea binadamu mwenzako au hata kumkosesha mwingine ni kumkosea Mungu mwenyewe. Mungu yuko kinyume kabisa na uchawi na matendo au tabia yoyote yenye vitendo vya kishirikina:Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu(Law 19:31). Na mtu yule atakayewaendea wenye pepo, na wachawi, ili kuzini pamoja nao, nitakaza uso wangu juu ya mtu yule, nitamtenga na watu wake. ... Tena mtu mume au mtu mke aliye na pepo, au aliye mchawi, hakika atauawa; watawapiga kwa mawe (Law 20:6, 27). Kwa maana mtu atendaye hayo [kuloga, kupandisha pepo au kuwaomba wafu] ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako (Kum 18:12). Uchawi ni uasi kwa Mungu. Kutenda au kushiriki uchawi ni kuvunja amri ya kwanza na ya msingi katika amri kumi za Mungu. Amri hii inasema:Mimi ni BWANA Mungu wako usiwe na miungu mingine ila mimi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 02/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/