Soma Biblia Kila Siku 02/2024Mfano
Maskini, watoto, wageni, wajane, na yatima ni makundi ya wanadamu yanayohitaji kutazamwa kipekee. Hawa wote wanahitaji kutendewa haki na wema (unaweza kulinganisha na Mt 25:35-42 kwa uelewa zaidi). Mungu anahusika sana na watu wanyonge. Watu wote waliokombolewa wanaonywa wasiwatendee wengine isivyo haki:Usimwonee mgeni, wala kumtendea jeuri; kwa kuwa ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri(m.21). Mungu amewaweka Wakristo popote walipo ili wachukue wajibu mzito wa upendo. Ni pamoja na kuwajali na kuwahudumia watu walio katikati yao ambao hawana makao, ni wafungwa au wanapungukiwa hata mahitaji ya lazima.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 02/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/