MsihangaikeMfano
Sababu ya Kuhangaika au Kuwa na Wasiwasi
Katika msitari wa 24, Yesu alisema: Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali. Na msitari wa 25, Yesu anaendelia kusema hivi: Kwa sababu hiyo, nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini.
Neno hili kwa hiyo ianzayo katika msitari wa 25, linamaanisha, kwa sababu hiyo. Basi, hili neno, kwa hiyo limeungana na wazo lililopo katika msitari wa 24. Hii ni kumaanisha kwamba kwa mistari hii miwili, Kristo alisema: Kwa sababu hamwezi kutumikia mabwana wawili ambao ni Mungu na Mali kwa wakati mmoja, msihangaike kwa sababu kama munahangaika, hamumtumikii Mungu, bali mnatumikia mali.
Kwa kweli, Kristo alikuwa anasema katika mistari hii miwili kwamba, tunapohangaika, tunaabudu fedha, sio Mungu, na tunaonyesha kuwa fedha zimechukua nafasi ya Mungu maishani mwetu, na kuwa miungu tunayoiabudu. Yaani, tunapohangaika au kuwa na wasiwasi, tunatenda dhambi ya kuabudu sanamu.
Sanamu ni kitu chochote ijapo tukipoteze, tungeona kwamba maisha hayana thamani tena kwa sababu tunahisi hicho kitu ndicho kinachotupa maana, kusudi, usalama, na kuridhika katika maisha.
Ukweli wa mambo ni kwamba, mwishowe, tutapoteza vitu vyote na fedha pia ikiwa tumeweka matumaini na imani yetu juu ya hayo kushinda Mungu. Tutapotea. Mungu pekee ndiye adumuye milele, na kwa sababu hiyo, kitu kimoja ambacho hatuwezi kukipoteza ni Mungu na uhusiano wetu naye, ambao utaendelea hadi milele na milele.
Basi, muhtasari wa pili ni kusema kwamba, katika kifungu hiki, Kristo alisema kuwa sababu tuna wasiwasi au tunahangaika iwe makusudi au bila kufahamu, mioyoni mwetu tumeruhusu fedha na mali kuwa sanamu zinazochukua nafasi ya kumwabudu Mungu ambaye ni hakika na imara na asiyeweza kufananishwa na fedha au mali ambazo tunaweza kuzipoteza.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Katika kitabu cha Mathayo 6:24-34 Kristo anaeleza jinsi Injili inadhihirisha sababu hasa tunakumbwa na wasiwasi au mahangaiko, na la muhimu zaidi, Kristo anatuwezesha kuelewa jinsi Injili inavyotuokoa kutokana na uwepo wa wasiwasi au mahangaiko.
More
Tungependa kuwashukuru Emmanuel Kwasi Amoafo kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://returningtothegospel.com/