Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

MsihangaikeMfano

Msihangaike

SIKU 5 YA 5

Msihangaike!

Katika Mathayo 8:20, Yesu akawaambia, Mbweha wana pango, na ndege wa angani wana viota; lakini Mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake. Hii ilikuwa kwa sababu Kristo alikuwa ameondoka nyumbani, na alikuwa ameacha kazi yake ya ufundi, na kuwa mhubiri msafiri. Tunajua kutoka Luka 8:1-3 kwamba, baada ya kuacha nyumba na biashara yake ya ufundi, Kristo sasa alitegemea wafuasi wake kifedha.

Hii inatuambia kwamba uaminifu wa Mungu katika kutosheleza mahitaji ya watu wake anavyotufunza Kristo katika Mathayo 6:24-34, ilikuwa kutokana na Kristo mwenyewe kumtegemea Mungu kwa mahitaji yake binafsi na kushuhudia uaminifu wa Baba yake wa Mbinguni. Kwa hivyo, katika kifungu hiki, Kristo hakuwa tu akifundisha jambo ambalo lilionekana kuwa zuri tu; bali alikuwa akifundisha kutokana na uzoefu wake yeye mwenyewe kama ukweli katika maisha yake.

Habari njema ya injili ni kwamba, katika Mathayo 27:46, Kristo, msalabani

Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Yeye alikuwa ameachwa na Baba yake, hivyo kwamba wakati sisi tukiweka imani yetu katika kile alichokifanya kwa ajili yetu pale msalabani, Baba yetu kamwe hatatuacha.

Warumi 8:32 inathibitisha hili kwa maneno haya: Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye? Mstari huu unatangaza kwamba, kwa msingi wa injili njema ya kazi ya Kristo iliyokamilishwa kwa ajili yetu msalabani, tunaweza kwa haki kumtarajia Baba yetu wa mbinguni kutosheleza mahitaji yetu yote ya kimwili.

The all things in Rom. 8:32 corresponds to the all these things of Christ in Matt. 6:33 when He declared that, but seek first His kingdom and His righteousness, and all these things will be given to you as well.

“Mambo hayo yote” katika Warumi 8:32 inalingana na “na hayo yote” aliyosema Kristo katika Mathayo 6:33 aliposema hivyo, bali utafuteni ufalme wake na haki yake, na hayo yote mtazidishiwa.

Kwa hivyo masomo haya matatu kutokana na mafunzo ya ibada hii, yawatie moyo, na ukweli wa injili ya Kristo iwaepushe kutokana na mahangaiko na wasiwasi mnapoendelea kuweka imani yenu kwa Mungu, ambaye hakumzuia Mwanawe wa pekee, bali alimtoa kwa ajili yenu, na basi kwa neema atawapa kila kitu mnachohitaji.

siku 4

Kuhusu Mpango huu

Msihangaike

Katika kitabu cha Mathayo 6:24-34 Kristo anaeleza jinsi Injili inadhihirisha sababu hasa tunakumbwa na wasiwasi au mahangaiko, na la muhimu zaidi, Kristo anatuwezesha kuelewa jinsi Injili inavyotuokoa kutokana na uwepo wa wasiwasi au mahangaiko.

More

Tungependa kuwashukuru Emmanuel Kwasi Amoafo kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://returningtothegospel.com/

Mipango inayo husiana