Soma Biblia Kila Siku 05/2024Mfano
Yohana Mbatizaji ni nabii wa mwisho wa Agano la Kale, tena ni mkuu kuliko manabii wengine, kwa sababu amepewa wajibu wa pekee wa kumtengenezea Bwana mwenyewe njia. Kazi ya Yohana ilileta uamsho mkubwa kwa Wayahudi, watu walimjia kwa wingi, kama ilivyoelezwa katika m.12:Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka. Lakini pamoja na Yesu yanaanza majira mapya ambayo ni kutimizwa kwa maneno yote ya manabii. Ni majira ya ufalme wa Mungu kukaribia kwetu.Aliye mdogo katika ufalme wa Mungu, maana yake ni mwanafunzi wa Yesu. Ndivyo anavyoeleza wazi katika Mt 10:42:Mtu awaye yote atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa ngaa kikombe cha maji ya baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, .... Yesu anamaanisha kuwa wanafunzi wake ni wakubwa kuliko Yohana.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa tano pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka, Yoeli na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/