Soma Biblia Kila Siku 05/2024Mfano
Kuna umoja kati ya Yesu na wafuasi wake. Umoja huu Yesu anaulinganisha na umoja wa kiukoo. Kwa hiyo kukubali kumwamini Yesu Kristo na kuwa mfuasi wake ni kukubali kuingia katika familia mpya, familia ya Yesu Kristo. Katika familia hii Mungu ni Baba yako, Yesu ni ndugu yako, na Wakristo wengine ni ndugu zako. Baadhi yao ni kama baba na mama wa kiroho kwako. Msingi wa umoja huu ni kufanya mapenzi ya Baba yetu ambayo jambo lake la kwanza ni kumwamini Mwana wake, Yesu Kristo. Yohana anafafanua jambo hili hivi katika 1 Yoh 3:23-24:Hii ndiyo amri yake, kwamba tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana sisi kwa sisi, kama alivyotupa amri. Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye, naye ndani yake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa tano pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka, Yoeli na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/