Soma Biblia Kila Siku 05/2024Mfano
Uharibifu kutokana na baa la nzige ni kitu kidogo tu ukilinganisha na hali itakayokuwepo wakati wa hukumu ya siku ya BWANA. Mkazo wa nabii ni kuwa hata kama nchi ingekuwa nzuri kama bustani ya Edeni, ikiingia katika hukumu ya BWANA itaachwa kama jangwa. Mungu anakaza jambo hilohilo katika Isa 13:10-13:Nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze.Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali; nitafanya wanadamu kuadimika kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dhahabu ya Ofiri.Kwa hiyo nitazitetemesha mbingu, na dunia itatikiswa itoke katika mahali pake, kwa sababu ya ghadhabu ya Bwana wa majeshi, na kwa sababu ya siku ya hasira yake kali.M.11 unaishia kwa kuuliza swali:Ni nani awezaye kuistahimili?Jibu ni kwamba hakuna anayeweza kushindana na Bwana anapotoa hukumu yake. Ni muhimu sana kwa sisi sote tukubali ujumbe wa Neno la Mungu na kutubu kwa moyo wa dhati ili tupate rehema ya Mungu siku hiyo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa tano pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka, Yoeli na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/