Soma Biblia Kila Siku 05/2024Mfano
Kuhusu maisha ya kiroho, Yoeli, anaeleza kuhusu hali mpya itakayotokea kwa watu wa Mungu. Roho Mtakatifu atawajilia na kuwaongoza. Hali mpya ya Roho Mtakatifu kumiminwa juu ya waamini ilitimia siku ya Pentekoste (kama una nafasi kusoma ilivyosimuliwa katika Mdo 2:14-21ukilinganisha na Yn 16:7-15). M.31-32 inaendelea kutoa ujumbe kwa habari ya hukumu ya siku ya Bwana na kuonyesha kuwa ukombozi upo kwa wale watakaoliitia jina la BWANA:Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo.Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la Bwana ataponywa; kwa kuwa katika mlima Sayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama Bwana alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao Bwana.Kwa upande mwingine hukumu itakuwepo kwa wote ambao hawakumtumainia BWANA. Hebu ujiulize wewe utakuwa upande gani?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa tano pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka, Yoeli na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/