Soma Biblia Kila Siku 05/2024Mfano
Kushuka kwa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste ndiko kuzaliwa kwa Kanisa. Lengo la kushuka kwake ni kuwawezesha wanafunzi kuwa mashahidi wa Yesu kwa ulimwengu mzima. Wanafunzi wote walikuwepo pamoja. Kulitokea matukio ya pekee, kama uvumi mkubwa wa upepo, ndimi za moto zilizosambaa, na wanafunzi kusema juu ya matendo makuu ya Mungu kwa lugha mbalimbali ambazo Wayahudi waliotoka sehemu nyingi za dunia walizifahamu. Ulikuwa mwujiza wa pekee. Wengi wakasikia Injili na kumwamini Yesu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa tano pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka, Yoeli na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/