Soma Biblia Kila Siku 05/2024Mfano
Maadui wa watu wa Mungu watapokea hukumu. Hukumu itaendana na namna walivyowatendea vibaya Israeli. Mataifa ya Tiro, Sidoni na Filisti yanatajwa kama maadui wa watu wa Mungu. Ni kweli, haya mataifa yamewatendea Waisraeli kwa ukatili. Wamewapigia kura watu wangu; na mtoto mwanamume wamemtoa ili kupata kahaba, na mtoto mwanamke wamemwuza ili kupata divai, wapate kunywa(m.3). Mtume Paulo anatukumbusha juu ya ujira kwa kila tendo, jema au baya.Ni haki mbele za Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi; na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi; wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake; katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu; watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake(2 The 1:6-9). “Bonde la Yehoshafati”au “Bonde la kukata maneno”ni mahali patakapotumika kutolea hukumu. Mataifa watajaribu kujipanga kwa vita. Lakini hakuna atakayeweza kushindana na BWANA.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa tano pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka, Yoeli na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/