Soma Biblia Kila Siku 05/2024Mfano
Kurarua vazi kwa mtu ambaye yuko katika hali ya kuomba na kufunga ni namna ya kuonyesha moyo uliopondeka na kujutia kosa. Nabii anawasihi wasifanye toba kwa ajili ya baa la nzige tu, ila toba yao ihusishe kujenga uhusiano mpya na Mungu. Nabii aliwaonya kwamba wakumbuke kuwa ipo siku ya BWANA ya kutoa hukumu kwa ulimwengu mzima. Toba yao itoke moyoni. Hayo ni maonyo kwetu pia. Toba yetu ianzie ndani mioyoni mwetu, kama Bwana anavyomwambia Samweli katika 1 Sam 16:7:Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo. BWANA ni mwenye rehema: Tukimrudia naye ataturudia sisi. Ndivyo Mungu anavyoahidi katika Zek 1:3:Nirudieni mimi, asema Bwana wa majeshi, nami nitawarudia ninyi, asema Bwana wa majeshi
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa tano pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka, Yoeli na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/