Soma Biblia Kila Siku 05/2024Mfano
Mungu anafanya upya agano lake na Waisraeli na kusema atawapigania ili waweze kumiliki nchi ile aliyowaahidi. Kuna wajibu pamoja na kupokea neema hiyo: Waisraeli wasiungane na wapagani wanaoishi hapo nchini wala kushiriki katika ibada zao za miungu. Sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu iwakumbushe wamekombolewa kutoka utumwani Misri na kuwa watu wa Mungu, basi wasikengeuke na kurudia maisha ya zamani. Tukimwamini Kristo, ni wenyeji wa mbinguni. Hivyo, usifuate mambo ya wenyeji wa ulimwengu huu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa tano pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka, Yoeli na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/