Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kueneza Habari Za Yesu Katika Mwaka WaMfano

Kueneza Habari Za Yesu Katika Mwaka Wa

SIKU 3 YA 5

"Sauti" inayofaa ya kutumia wakati wa kuenea habari za Yesu

Kuzungumza na marafiki na familia zetu kuhusu imani kunaweza kuwa na changamoto. Mara nyingi, mazungumzo hayo yanaweza kugeuka na kuwa mzozano na watu wanaweza kukasirika.

Miaka mingi iliyopita, mtafiti wa kijamii kule Australia aliandika kwamba tunapopinga moja kwa moja maoni ya mtu mwingine kuhusu ulimwengu, inawezekana kwamba tutatia nguvu msimamo wake badala ya kubadilisha mawazo yake. 

Je, umeelewa hiyo? Kimsingi ni kwamba...kupinga imani ya mtu kuna uwezekano mkubwa wa kumtorosha mtu huyo badala ya kumhimiza abadilike!

Kwa hivyo, hiyo ina maana gani kwetu? Ina maana kwamba sauti ni muhimu sana, na mazungumzo yetu pia ni muhimu. Mara nyingi tunaweza kufikiria kwamba kushinda katika mzozano kunaweza kumbadilisha mtu, au mwishowe kutamhimiza kumkubali Yesu. Petro anaandika katika maandiko tunayoyasoma kwamba, tunapotoa jawabu tunapaswa kufanya hivyo kwa upole na heshima, na kwamba cha muhimu ni kudumisha urafiki, siyo kuwafukuza watu kwa majibu makali na ukosefu wa heshima.

Hata kunapotokea ugomvi, jukumu letu ni kuwa wawakilishi wa Yesu Kristo wenye upendo na unyenyekevu, huku tukifahamu kwamba si uwezo wetu wa kiakili unaowaleta watu kwake, bali ni mtazamo wetu.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Kueneza Habari Za Yesu Katika Mwaka Wa

Mwito wa kila Mkristo ni kueneza habari za Yesu zenye uwezo wa kubadilisha maisha na jinsi Yesu anavyoweza kumbadilisha kila mtu kikamilifu. Mpango huu wa siku tano unatoa mwongozo halisi kuhusu jinsi unavyoweza kuitikia mwito huu kila siku na uone Yesu akibadili maisha ya walio karibu nawe wanaohitaji kumfahamu.

More

Tungependa kumshukuru YesI kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://yesheis.com/

Mipango inayo husiana