Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kueneza Habari Za Yesu Katika Mwaka WaMfano

Kueneza Habari Za Yesu Katika Mwaka Wa

SIKU 5 YA 5

Namna ya 'kujikwamua kiinjili'

Kuna sababu anuwai zinazotufanya tusieneze habari za Yesu kwa marafiki zetu. Tunaweza kuwa na hofu ya kukataliwa, hofu ya kuharibu urafiki wetu, au hofu kwamba hatuna majibu ya kutosha.

Pengine hata tumejaribu "kueneza injili" mara moja au mara mbili hapo awali, lakini tukagundua kwamba ilikuwa vigumu sana au ya kufedhehesha, kwa hivyo tukafa moyo.

Tunapojipata kwamba "tumekwama kiinjili" kwa njia hii, wakati mwingine ni vyema kuangalia kilichotuchochea kueneza injili tangu mwanzo. 

Askofu mkuu Justin Webly hivi majuzi alisema: "Kujitolea kueneza injili ... hutokana na upendo, si kutokana na woga. Hutokana na kuwa mtiifu kwa Kristo, si kutokana na wasiwasi wa idadi ya hivi majuzi ya wanaohudhuria kanisa."

Fahamu kwamba, kugawana imani yetu na wengine hakukustahili kuwa jukumu gumu tunalofanya kutokana na hofu au wajibu. Badala yake, Yesu anataka tueneze injili kutokana na upendo wetu kwake na huruma yetu kwa wengine. 

Tunaporuhusu upendo wa Mungu kukua ndani yetu, tukiziacha njia zetu za zamani na kupokea maisha mapya, moja kwa moja upendo huo huwafikia wengine walio karibu nasi!

Wakati mwingine utakapojipata "umekwama kiinjili," zingatia zaidi kumpenda yule mtu ambaye roho wa Mungu anakushawishi umnenee kuhusu habari zake. Hatujui kamwe yale ambayo Mungu tayari anayafanya katika maisha ya watu walio karibu nasi. Lakini tunaweza kubadilisha mitazamo yetu kuhusiana na uinjilisti ili tuwe tunapatikana kila wakati Mungu anapotaka kututumia.

Kwa hivyo tunapokaribia mwisho wa mpango huu na tunapofikiria kuhusu mwito huu wa ajabu wa kueneza habari za Yesu kwa wale walio karibu nasi, anza kujiuliza "sababu za kueneza injili ni zipi?" na utagundua kwamba upendo wa Yesu utasisimuka ndani yako na kutawala juu ya hofu yetu na vikwazo vinavyotuzuia.

KMbona usieneze  Kristo sasa hivi Kwa kutuma video  kupitia  App ya yesHEis ?

siku 4

Kuhusu Mpango huu

Kueneza Habari Za Yesu Katika Mwaka Wa

Mwito wa kila Mkristo ni kueneza habari za Yesu zenye uwezo wa kubadilisha maisha na jinsi Yesu anavyoweza kumbadilisha kila mtu kikamilifu. Mpango huu wa siku tano unatoa mwongozo halisi kuhusu jinsi unavyoweza kuitikia mwito huu kila siku na uone Yesu akibadili maisha ya walio karibu nawe wanaohitaji kumfahamu.

More

Tungependa kumshukuru YesI kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://yesheis.com/

Mipango inayo husiana