Soma Biblia Kila Siku 08/2024Mfano
Sedekiaakafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, Mungu wake; wala hakujinyenyekesha mbele ya Yeremia nabii aliponena kwa kinywa cha Bwana(2 Nya 36:12), baliakamwasi mfalme wa Babeli(2 Fal 24:20). Nabii Yeremia alitabiri kuwa ikiwa Wayuda wangeungana na Misri dhidi ya Babeli itaamsha tu hasira ya Wababeli, na baadaye wangerudi kwa nguvu na kuiteka Yuda. Utabiri huo ulibezwa na wenyeji wa Yerusalemu, wakamfunga Yeremia gerezani (tafuta mwenyewe Yer 37:1-38:28 ili kusoma habari hizi).Ila Neno la Mungu halifungwi. Unabii wa nabii ukatimia baada ya muda mfupi. Hii itufundishe kutopingana na watumishi waliotumwa na Mungu kutuonya tunapokosea.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 08/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Nane pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Wafalme na 1 Timotheo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz