Yesu Ni Nani?Mfano
Yeye ndiye Uzima.
‘Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.’ (Yohana 1:4).
Mwanzo wangu ulikuwa katikati au huenda ulikuwa mwishoni. Kabla sijaja, tayari nilikuwepo. Baada yangu, nitakuwepo.
Mimi ni sehemu ya picha kubwa. Ya kila kitu. Mtiririko wa mpango wa Mungu. Ndivyo yalivyo maisha yetu kutoka katika mtazamo wa milele, mtazamo wetu unapopanuka, na mawazo yetu kwenda kufikiria yote ya muda na nafasi. Tunaweza kuona jinsi malezi ya Mungu kwetu yameenda zaidi kuliko tunavyoweza kufikiria katika maisha yetu ya kila siku.
Yohana anaandika,‘Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu (Yohana 1:4). Umilele wa Mungu unajumuisha wako na wangu sasa, jambo linalotupa sisi mahali imara pa ukamilifu pa kuanzia tunapopahitaji kila siku. Lakini nalo vile vile ni kubwa zaidi ya tunavyoweza kuhesabu au kuelewa. Halina mwisho. Halina kikomo.
Katika Yesu, Mungu anasogelea ‘wanadamu wote’. Katika hali zote mbalimbali, mazingira, desturi au nyakati, Yeye anakuwa uzima, kwa kila mmoja. Kwa sababu ‘fadhili zake ni za milele’(1 Mambo ya Nyakati 16:34).
Katika sehemu mbalimbali duniani, tunaweza tukawa na mila mbalimbali za Ujio. Katika mila yetu ya Kiswidishi, Jumapili ya tatu katika Ujio inamhusu Yohana Mbatizaji tu na ujumbe wa Kristo anayekuja. Sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Itengenezeni njia ya Bwana, yanyoosheni mapito yake’ (Luka 3:4).
Nami nafikiria kuhusu ‘nyikani’ ndani ya jamii yangu mwenyewe na majirani. Mahali ambapo watu wenye kuchoshwa wakati wa ujio wanahitaji kusikia kwamba kuna uzima. Katika ukamilifu wake. Kwa ajili ya kila mmoja. Vile vile kwa watu ambao hatuwaelewi au hata hatuwataki. Nuru ya wanadamu wote. Yesu. Nami nasikia msukumo wa kwenda ‘nyikani’ kuzunguka nyuma mahali watu wamechoshwa wanahitaji nuru katika handaki na kushirikishwa habari. Kuelezea hadithi kuu ya uzima tumaini, maana na kusudi tulilopewa katika Yesu. Ujumbe wa milele. Kwa ajili ya kila kizazi.
Ni kwa njia ipi mimi nakumbatia maisha ya Yesu katika mazingira yangu binafsi? Kuna jambo ambalo nataka kuwa tofauti, kama ndivyo, mpango wangu ni upi wa kulipata hilo?
-
Mungu, nasikia kizunguzungu. Je, kweli unamaanisha msamaha wako ni wa milele? Faraja yako haina kikomo? Majibu yako na uvumilivu wako hauchoki? Nasimama nikiwa nimeishiwa maneno na nashangazwa. Mimi ni sehemu...hata pungufu kuliko sehemu ya darubini, lakini bado napendwa na kukubalika kikamilifu, sehemu ya milele ya Mungu, kwa wakati huu, nikiwa katika mchakato wa kupata? Nina kizunguzungu cha shukrani! Nisaidie nipate njia ya kumshirikisha mwengine habari hii kuu leo. Nisaidie niipate sehemu yangu ‘nyikani’ niandae njia kwa ajili yako!
Amina
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Tunapoingia Ujio, tukisubiri na kujiandaa kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu, tukiiandaa mioyo yetu kwa ajili ya Krismasi, maneno ya Mtakatifu Yohana yanatutangazia hali ya uungu na uwepo wa milele wa Yesu, aliyekuja ‘kusimamisha hema lake’ kati yetu.
More
Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org