Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yesu Ni Nani?Mfano

Yesu Ni Nani?

SIKU 4 YA 5

Yeye ndiye Nuru.

‘Nayo Nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.’. (Yohana 1:5)

Tunapokuwa katika nyumba yenye giza na tukasikia kelele tusiyoitambua, kwa hisia tu sisi huwasha taa ili tuweze kuona na tuonekane. Nuru huangaza kwenye giza na hutusaidia tuone kila kitu wazi. Inazungumzia kuhusu usalama na uhakika, hekima na uelewa.

Nuru ina thamani safi sana, na yakuvutia. Inadhihirisha wema, kweli na utakatifu. Palipo na nuru, pana uzima. Palipo na nuru, giza haliwezi kudumu hapo.

Katika dunia hii, kuna giza jingi mno. Kuna dhambi na kuna uovu. Kila moyo wa mwanadamu unamenyana na vifungo vya dhambi, pamoja na moyo wa majivuno, mifumo ya mawazo yasiyo bora, na dhambi za tabia zinazoonekana kuwa ngumu kuachana nazo. Lakini nuru ina uwezo na inaweza kufika mbali. Hakuna kitu wala mahali penye giza nene nuru ishindwe kuangaza.

Yesu alisema: ‘...Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.’ (Yohana 8:12).

Yesu ndiye aletaye nuru, yeye afukuzaye giza la dhambi kutoka kwa wale wanaomfuata. Yeye atuletaye kwenye nuru, aangazaye hatua yetu inayofuata na kutuonyesha njia. Yeye ndiye nuru ya ulimwengu.

Kama wafuasi wake Yesu, waliojazwa Roho Mtakatifu, tunaweza kuangaza nuru yake kwenye giza la dunia hii kupitia kwa maneno yetu na matendo yetu, tukiwasaidia wengine waone na waje nao wamfahamu yeye vile vile.

Ina maana gani kwako kwamba Yesu ni nuru? Ulifikaje kutambua nuru hii kuu? Nuru ya Yesu imefukuza namna gani giza litoke maishani mwako?

-

Mpendwa Bwana, asante kutuonyesha nuru yako na kutusaidia tutembee katika nuru yako. Tafadhali tusaidie tuangaze nuru hii na tuwaongoze wengine watoke kwenye giza waingie kwenye nuru.

Katika jina la Yesu naomba.

Amina

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Yesu Ni Nani?

Tunapoingia Ujio, tukisubiri na kujiandaa kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu, tukiiandaa mioyo yetu kwa ajili ya Krismasi, maneno ya Mtakatifu Yohana yanatutangazia hali ya uungu na uwepo wa milele wa Yesu, aliyekuja ‘kusimamisha hema lake’ kati yetu.

More

Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org