Soma Biblia Kila Siku 12/2024Mfano
Zaburi hii inafurahia ukuu wa Mungu na kwamba ukuu wake umo Yerusalemu.Bwana ndiye aliye mkuu, Na mwenye kusifiwa sana. Katika mji wa Mungu wetu, Katika mlima wake mtakatifu(m.1). Siri ya uwepo wa Mungu Yerusalemu ni hekalu lake. Ndivyo watu wake wanavyokumbuka katika m.9:Tumezitafakari fadhili zako, Ee Mungu, Katikati ya hekalu lako. Hekaluni Mungu alijifunua,katika majumba yake Amejijulisha kuwa ngome(m.3). Hili lilikuwa kusudi la Sulemani kulijenga hekalu, kama anavyosema katika 1 Fal 8:13,Nimekujengea nyumba ya kukaa, iwe mahali pa makao yako milele. Hivyo Wayahudi walipokutana na Mungu hekaluni katika roho na kweli, kwao ilileta baraka. Mungu aliwapigania vitani.Maana, tazama, wafalme walikusanyika; Walipita wote pamoja. Waliona, mara wakashangaa; Wakafadhaika na kukimbia(m.4-5). Sisi watu wa Mungu kipindi cha Agano Jipya tunapata baraka iyo hiyo, si katika hekalu fulani bali kwa Yesu. Kwa Yesu uko salama. Ujikabidhi kwake katika yale yanayokutisha na kukupa mashaka.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na mbili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz