Soma Biblia Kila Siku 12/2024Mfano
Zaburi hii inahusu uhusiano kati ya mwenye haki na asiye na haki. Daudi anaeleza hasa ule uchungu anaopata mwenye haki anapoona mtu asiye na haki akifanikiwa katika mambo yake. Mwenye haki asijaribu kujipatia haki na kushinda kwa kutumia silaha na tabia ya asiye na haki. Badala yake, amkabidhi Bwana njia yake na kuwa na upole!Usikasirike kwa sababu ya watenda mabaya, usiwahusudu ... ukae kimya mbele za Bwana, nawe umngoje kwa saburi ... wenye upole watairithi nchi(m.1, 7 na 11).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na mbili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz