Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 12/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 12/2024

SIKU 30 YA 31

Kwa njia gani inawezekana kwa mwenye dhambi kukaa kivulini mwa Bwana? Mfalme Daudi anashuhudia:Heri aliyesamehewa dhambi, Na kusitiriwa makosa yake. Heri Bwana asiyemhesabia upotovu, Ambaye rohoni mwake hamna hila. Niliponyamaza mifupa yangu ilichakaa Kwa kuugua kwangu mchana kutwa. Kwa maana mchana na usiku Mkono wako ulinilemea. Jasho langu likakauka hata nikawa Kama nchi kavu wakati wa kaskazi. Nalikujulisha dhambi yangu, Wala sikuuficha upotovu wangu. Nalisema, Nitayakiri maasi yangu kwa Bwana, Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu(Zab 32:1-5). Ushuhuda wa Mtume Yohana hufanana. Anasema:Tukienenda nuruni, kama [Mungu] alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote(1 Yoh 1:7). Katika somo la leo tunaambiwa kwamba anayekaa hivyo kivulini mwa Bwana, kwake maovu ya usiku hayatampata wala ya mchana. Wala yaliyofichwa na yanayoonekana. Hata ukiona wengi wanaanguka, hayo yote hayatakukaribia wewe. Katika Agano Jipya kuna mistari inayofanana sana na mistari hii. Tafuta mwenyewe Rum 8:31-39 ukaisome. Ukilinganisha mistari hii yote, utaona kwamba Mungu ni yeye yule katika Agano la Kale na Agano Jipya. Upendo wake ni katika Kristo, na ni upendo huu tunaoona katika Zab 91.

siku 29siku 31

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 12/2024

Soma Biblia Kila Siku 12/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na mbili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz