Yohane 3

3
Yesu na Nikodemo
1Kulikuwa na kiongozi mmoja Myahudi, wa kikundi cha Mafarisayo, jina lake Nikodemo.#3:1 Nikodemo: Anatajwa tu katika Injili ya Yohane (7:50-52; 19:39-42). Kwamba Nikodemo alimjia Yesu usiku inadokezea kwamba hakutaka kuonekana. Huyu Nikodemo anatajwa tu katika Injili hii ya Yohane (7:50). 2Siku moja Nikodemo alimwendea Yesu usiku, akamwambia, “Rabi, tunajua kwamba wewe ni mwalimu uliyetumwa na Mungu, maana hakuna mtu awezaye kufanya ishara unazozifanya Mungu asipokuwa pamoja naye.”
3 # 3:3-4 Ni kawaida katika Injili ya Yohane kutumia maneno au mafungu ya maneno kwa maana ya juu zaidi kuliko ile inayoeleweka kwa kawaida ambayo wasikilizaji wake hawawezi kuelewa. Baada ya mafundisho ya Yesu baadhi wanafikia imani (2:21-22; 4:10-15,32-34; 11:11-13; 13:6-15,33-38; 14:2-9), wengine wanabaki na hali yao ya kutokuamini (6:32-35,52-58; 7:33-33-36; 8:21-24,31-33,51-53,56-59). Yesu akamwambia, “Kweli nakuambia, mtu asipozaliwa tena#3:3 Asipozaliwa tena: Au, “Asipozaliwa upya”. Neno la Kigiriki pia lina maana ya “kutoka juu” Taz k.m. Yoh 1:13; 2Kor 5:17 (kiumbe kipya); Gal 6:15 (kiumbe kipya); Tito 3:5; 1Pet 1:3,23,39). hataweza kuuona ufalme wa Mungu.”#3:3 Ufalme wa Mungu: Msemo huu wapatikana hapa tu katika Injili ya Yohane na katika aya ya 5. Ufalme wa Mungu sio tu mahali fulani. Ufalme wa Mungu huwa wakati Mungu anapotawala na watu wanafuata matakwa yake, kama vile kuwatumikia wengine na kutangaza habari njema juu ya Yesu. 4Nikodemo akamwuliza, “Mtu mzima awezaje kuzaliwa tena? Hawezi kuingia tumboni mwa mama yake na kuzaliwa tena!” 5Yesu akamjibu, “Kweli nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na Roho,#3:5 Mtu asipozaliwa kwa maji na Roho: Baadhi wanafikiri “maji” hapa linatumiwa kwa maana kuzaliwa kimwili, hali “Roho” linatumika kwa maana ya kuzaliwa kiroho. Wengine wafikiri “maji” linahusu ubatizo wa Yohane, hali “Roho” linahusu zawadi ya Yesu Kristo ya Roho Mtakatifu. Taz pia 1:33 maelezo. hawezi kamwe kuingia katika ufalme wa Mungu. 6Mtu huzaliwa kimwili kwa baba na mama, lakini huzaliwa kiroho kwa Roho. 7Usistaajabu kwamba nimekuambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8Upepo huvuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda. Ndivyo ilivyo kwa mtu aliyezaliwa kwa Roho.”#3:6-8 Upepo …Roho: Katika Kigiriki maneno “upepo” na “roho” ni neno lile lile moja. Hivyo wafafanuzi wengine wanaona hapa namna au mtindo wa “mchezo wa maneno” unaotumika mara kwa mara kufundisha mambo muhimu. Kuzaliwa kiroho ni hali ambayo haiwezi kuonekana kwa macho, ni kama fumbo.
9Nikodemo akamwuliza, “Mambo haya yanawezekanaje?” 10Yesu akamjibu, “Je, wewe ni mwalimu katika Israeli na huyajui mambo haya? 11Kweli nakuambia, sisi twasema tunayoyajua na kushuhudia tuliyoyaona, lakini nyinyi hamkubali ujumbe wetu. 12Ikiwa nimewaambieni mambo ya kidunia nanyi hamniamini, mtawezaje kuamini nikiwaambieni mambo ya mbinguni? 13Hakuna mtu aliyepata kwenda juu mbinguni isipokuwa Mwana wa Mtu,#3:13 Mwana wa Mtu: Mwishoni mwa aya hii baadhi ya hati za kale zina: “ambaye yuko mbinguni”. ambaye ameshuka kutoka mbinguni.
14“Kama vile Mose alivyomwinua juu nyoka wa shaba kule jangwani, naye Mwana wa Mtu atainuliwa#3:14 Mwana wa Mtu atainuliwa: Yesu alikuwa na maana ya “kuinuliwa juu ya msalaba” hivyo kwamba yeyote aliyemwamini angeokolewa kutoka kifo. juu vivyo hivyo, 15ili kila anayemwamini awe na uhai wa milele.#3:15 Anayemwamini awe na uhai wa milele: Uhai ni zawadi kuu mno ambayo Mungu anawajalia watu. Uhai huo hautatoweka na kifo (Yoh 11:25) na ndiyo maana mara nyingi unaitwa “uhai wa milele”. Uhai huo unapatikana tu kwa imani katika Yesu Kristo (Yoh 3:16,36), sasa na baadaye (Yoh 5:24). Umuhimu wa dhana hii au wazo hili ni kama ule wa “Ufalme wa Mungu” unaotajwa katika Injili za sunoptiki (rejea Yoh 5:24; 6:35-54; 20:31). 16Maana Mungu aliupenda ulimwengu hivi hata akamtoa Mwana wake wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uhai wa milele. 17Maana Mungu hakumtuma Mwanae ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali aukomboe.
18“Anayemwamini Mwana hahukumiwi; asiyemwamini amekwisha hukumiwa, kwa sababu hakumwamini Mwana wa pekee wa Mungu. 19Na hukumu yenyewe ndiyo hii: Mwanga umekuja ulimwenguni lakini watu wakapenda giza kuliko mwanga, kwani matendo yao ni maovu. 20Kila mtu atendaye maovu anauchukia mwanga, wala haji kwenye mwanga, maana hapendi matendo yake maovu yamulikwe. 21Lakini mwenye kuuzingatia ukweli huja kwenye mwanga, ili matendo yake yaonekane yametendwa kwa kumtii Mungu.”
Yesu na Yohane Mbatizaji
22Baada ya hayo, Yesu alifika mkoani Yudea pamoja na wanafunzi wake. Alikaa huko pamoja nao kwa muda, akibatiza watu. 23Yohane pia alikuwa akibatiza watu huko Ainoni, karibu na Salemu,#3:23 Ainoni, karibu na Salemu: Vijiji ambavyo huenda vilikuwa kaskazini mwa Yudea katika bonde la mto Yordani. maana huko kulikuwa na maji mengi. Watu walimwendea, naye akawabatiza. 24(Wakati huo Yohane alikuwa bado hajafungwa gerezani.)
25Ubishi ulitokea kati ya baadhi ya wanafunzi wa Yohane na Myahudi mmoja kuhusu desturi za kutawadha. 26Basi, wanafunzi hao wakamwendea Yohane na kumwambia, “Mwalimu, yule mtu aliyekuwa pamoja nawe ng'ambo ya Yordani na ambaye wewe ulimshuhudia, sasa naye anabatiza, na watu wote wanamwendea.” 27Yohane akawaambia, “Mtu hawezi kuwa na kitu asipopewa na Mungu. 28Nanyi wenyewe mwaweza kushuhudia kuwa nilisema: ‘Mimi siye Kristo, lakini nimetumwa ili nimtangulie!’ 29Bibi arusi ni wake bwana arusi, lakini rafiki yake bwana arusi, anayesimama na kusikiliza, hufurahi sana anapomsikia bwana arusi akisema. Ndivyo furaha yangu ilivyokamilishwa. 30Ni lazima yeye azidi kuwa maarufu, na mimi nipungue.”
Anayekuja kutoka mbinguni
31Anayekuja kutoka juu ni mkuu kuliko wote; atokaye duniani ni wa dunia, na huongea mambo ya kidunia. Lakini anayekuja kutoka mbinguni ni mkuu kuliko wote. 32Yeye husema yale aliyoyaona na kuyasikia, lakini hakuna mtu anayekubali ujumbe wake. 33Lakini mtu yeyote anayekubali ujumbe wake anathibitisha kwamba Mungu ni kweli. 34Yule aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu, maana Mungu humjalia mtu huyo Roho wake bila kipimo. 35Baba anampenda Mwana#3:35 Baba anampenda Mwana: Tazama 13:3; Mat 11:27; 28:19; Luka 10:22. na amemkabidhi vitu vyote. 36Anayemwamini Mwana anao uhai wa milele; asiyemwamini Mwana#3:36 Anayemwamini …asiyemwamini Mwana: Hapa ni dhahiri, kutokana na mazingira ya makala hii ambayo inasema ghadhabu ya Mungu inampata yule “asiyemwamini”, ni dhahiri kwamba neno “asiyemwamini” linajumuisha wazo la “kutokumtii” au wazo la “kumuasi”. hatakuwa na uhai wa milele, bali ghadhabu ya Mungu hubaki juu yake.

ప్రస్తుతం ఎంపిక చేయబడింది:

Yohane 3: BHNTLK

హైలైట్

షేర్ చేయి

కాపీ

None

మీ పరికరాలన్నింటి వ్యాప్తంగా మీ హైలైట్స్ సేవ్ చేయబడాలనుకుంటున్నారా? సైన్ అప్ చేయండి లేదా సైన్ ఇన్ చేయండి