Logo ng YouVersion
Hanapin ang Icon

Mwanzo 17

17
Ishara ya agano
1 # Mwa 5:22; Ayu 1:1 Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na tisa, BWANA akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu. 2#Gal 3:17,18 Nami nitafanya agano langu nawe, nami nitakuzidishia sana. 3#Kut 3:6 Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, 4Hili ndilo agano langu nawe, utakuwa baba wa mataifa mengi, 5#Rum 4:17 wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Abrahamu,#17:5 Abrahamu: Abrahamu kwa maana ya ‘baba wa wengi’. kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi. 6Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako. 7#Lk 1:55; Mwa 26:24; 28:13; Ebr 11:16; Rum 9:7-9 Agano langu nitalifanya imara kati yangu na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako. 8#Mdo 7:5; Kut 6:7; 29:45; Law 26:12; Kum 4:37; 14:2; 26:18; Zab 48:14; Ufu 21:7 Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayokaa kama mgeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao.
9 # Zab 25:10 Mungu akamwambia Abrahamu, Nawe ulishike agano langu, wewe, uzao wako na vizazi vyao. 10#Mdo 7:8; Rum 4:11 Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati yangu nawe, na uzao wako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa. 11#Mdo 7:8; Rum 4:11; Gal 6:15 Mtatahiriwa nyama ya magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na ninyi. 12#Lk 2:21; Yn 7:22 Katika vizazi vyako vyote, kila mtoto wa kiume miongoni mwenu atatahiriwa akiwa na umri wa siku nane, awe mtumishi aliyezaliwa katika nyumba yako au uliyemnunua kwa fedha zako japo hakuwa wa uzao wako. 13Mzaliwa nyumbani mwako, na mnunuliwa kwa fedha yako, lazima atahiriwe; na agano langu litakuwa katika mwili wenu, kuwa agano la milele. 14#Kut 4:24; Yos 5:2-7 Na mwanamume mwenye govi asiyetahiriwa nyama ya govi lake, mtu yule atatengwa na watu wake; amelivunja agano langu.
15Mungu akamwambia Abrahamu, Sarai mkeo, hutamwita jina lake Sarai, kwa kuwa jina lake litakuwa Sara. 16#Mwa 18:10; 21:1 Nami nitambariki, na tena nitakupa mwana kwake, naam, nitambariki, naye atakuwa mama wa mataifa, na wafalme wa makabila ya watu watatoka kwake. 17#Mwa 18:12; 21:6,7 Ndipo Abrahamu akaanguka kifudifudi akacheka, akasema moyoni, Je! Mtu wa umri wa miaka mia moja, kwake atazaliwa mtoto? Naye Sara mwenye umri wa miaka tisini atazaa? 18Abrahamu akamwambia Mungu, Lau kwamba Ishmaeli angeishi mbele yako. 19#Mwa 18:10; 21:2; Gal 4:28-31 Mungu akasema, Sivyo, lakini Sara mkeo atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Isaka. Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake baada yake. 20#Mwa 16:10; 21:18; 25:12-16 Kuhusu Ishmaeli nimekusikia, nimembariki na nitamzidisha na kumwongeza sana. Atakuwa baba wa watawala kumi na wawili, na atakuwa na taifa kuu. 21#Mwa 21:2 Bali agano langu nitalifanya imara kwa Isaka, ambaye Sara atakuzalia majira kama haya mwaka ujao. 22#Mwa 18:33; 35:9-15 Mungu alipomaliza kusema naye, akaondoka kwa Abrahamu.
23 # Mwa 17:9 Abrahamu akamtwaa Ishmaeli mwanawe, na wote waliozaliwa nyumbani mwake, na wote walionunuliwa kwa fedha yake, wanaume wote wa watu wa nyumba ya Abrahamu, akawatahiri nyama ya magovi yao siku ile ile, kama Mungu alivyomwambia.
24Naye Abrahamu alikuwa mwenye umri wa miaka tisini na tisa alipotahiriwa nyama ya govi lake. 25Na Ishmaeli mwanawe alikuwa mtu wa miaka kumi na mitatu, alipotahiriwa nyama ya govi lake. 26#Zab 119:60 Siku ile ile akatahiriwa Abrahamu na Ishmaeli mwanawe. 27#Mwa 14:14; 18:19 Na watu wote wa nyumba yake, wazaliwa nyumbani, na wanunuliwa kwa fedha katika mkono wa mgeni, wakatahiriwa pamoja naye.

Kasalukuyang Napili:

Mwanzo 17: RSUVDC

Haylayt

Ibahagi

Kopyahin

None

Gusto mo bang ma-save ang iyong mga hinaylayt sa lahat ng iyong device? Mag-sign up o mag-sign in