Mwanzo 13
13
Abramu Na Lutu Watengana
1 Hivyo Abramu akakwea kutoka Misri kwenda Negebu, yeye na mkewe na kila kitu alichokuwa nacho, pia Lutu akaenda pamoja naye. 2 Wakati huo Abramu alikuwa tajiri sana wa mifugo, fedha na dhahabu.
3 Kutoka Negebu, akapita mahali hadi mahali, hadi akafika Betheli, mahali hapo ambapo mwanzoni alipiga hema lake kati ya Betheli na Ai 4 hapo ambapo alikuwa amejenga madhabahu ya kwanza. Huko Abramu akaliitia jina la bwana.
5 Basi Lutu, ambaye alikuwa anafuatana na Abramu, alikuwa pia na makundi ya mbuzi, kondoo, ng’ombe na mahema. 6 Lakini nchi haikuwatosha kukaa pamoja kwa ajili ya wingi wa mali zao. 7 Ukazuka ugomvi kati ya wachunga mifugo wa Abramu na wale wa Lutu. Wakati huo, Wakanaani na Waperizi ndio waliokuwa wenyeji wa nchi hiyo.
8 Hivyo Abramu akamwambia Lutu, “Pasiwe na ugomvi wowote kati yangu na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wako, kwa kuwa sisi ni ndugu. 9 Je, nchi yote haiko mbele yako? Tutengane. Kama ukielekea kushoto, nitakwenda kulia; kama ukielekea kulia, mimi nitakwenda kushoto.”
10 Lutu akatazama akaona lile bonde lote la Yordani kuwa lilikuwa na maji tele, kama bustani ya bwana, kama nchi ya Misri, kuelekea Soari. (Hii ilikuwa kabla bwana hajaharibu Sodoma na Gomora.) 11Hivyo Lutu akajichagulia bonde lote la Yordani, akaelekea upande wa mashariki. Watu hao wawili wakatengana: 12 Abramu akaishi katika nchi ya Kanaani, wakati Lutu aliishi miongoni mwa miji ya lile bonde na kupiga mahema yake karibu na Sodoma. 13 Basi watu wa Sodoma walikuwa waovu, wakifanya sana dhambi dhidi ya bwana.
14 Baada ya Lutu kuondoka bwana akamwambia Abramu, “Ukiwa hapo ulipo, inua macho yako utazame kaskazini na kusini, mashariki na magharibi. 15 Nchi yote unayoiona nitakupa wewe na uzao wako hata milele. 16 Nitaufanya uzao wako uwe mwingi kama mavumbi ya nchi, hivyo kama kuna yeyote awezaye kuhesabu mavumbi, basi uzao wako utahesabika. 17 Ondoka, tembea katika marefu na mapana ya nchi, kwa maana ninakupa wewe.”
18 Basi Abramu akaondoa mahema yake, akaenda kuishi karibu na mialoni ya Mamre huko Hebroni, huko akamjengea bwana madhabahu.
Kasalukuyang Napili:
Mwanzo 13: NMM
Haylayt
Ibahagi
Kopyahin
Gusto mo bang ma-save ang iyong mga hinaylayt sa lahat ng iyong device? Mag-sign up o mag-sign in
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018 by Biblica, Inc.
Used with permission.
All rights reserved worldwide.