1
Luka 6:38
BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA
Wapeni wengine wanavyohitaji, nanyi mtapewa. Naam, mtapokea mikononi mwenu kipimo kilichojaa, kikashindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika. Kwa maana kipimo kilekile mnachotumia kwa wengine ndicho atakachotumia Mungu kwenu.”
موازنہ
تلاش Luka 6:38
2
Luka 6:45
Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutoka katika hazina bora iliyomo moyoni mwake; na mtu mbaya hutoa yaliyo mabaya kutoka katika hazina mbaya iliyo moyoni mwake, kwa maana mtu huongea kutokana na yale yaliyojaa moyoni mwake.
تلاش Luka 6:45
3
Luka 6:35
Ila nyinyi wapendeni maadui zenu na kuwatendea mema; kopesheni bila kutazamia kurudishiwa, na tuzo lenu litakuwa kubwa, nanyi mtakuwa watoto wa Mungu aliye juu. Kwa maana yeye ni mwema kwa wale wasio na shukrani na walio wabaya.
تلاش Luka 6:35
4
Luka 6:36
Muwe na huruma kama Baba yenu alivyo na huruma.
تلاش Luka 6:36
5
Luka 6:37
“Msiwahukumu wengine, nanyi hamtahukumiwa; msiwalaumu wengine, nanyi hamtalaumiwa; wasameheni wengine, nanyi mtasamehewa.
تلاش Luka 6:37
6
Luka 6:27-28
“Lakini nawaambieni nyinyi mnaonisikiliza, wapendeni maadui zenu, watendeeni mema wale wanaowachukieni. Watakieni baraka wale wanaowalaani, na waombeeni wale wanaowatendea vibaya.
تلاش Luka 6:27-28
7
Luka 6:31
Jinsi mnavyotaka watu wawatendee nyinyi, watendeeni wao vivyo hivyo.
تلاش Luka 6:31
8
Luka 6:29-30
Mtu akikupiga shavu moja mgeuzie pia la pili. Mtu akikunyanganya koti lako mwachie pia shati lako. Yeyote anayekuomba mpe, na mtu akikunyanganya mali yako usimtake akurudishie.
تلاش Luka 6:29-30
9
Luka 6:43
“Mti mzuri hauzai matunda mabaya, wala mti mbaya hauzai matunda mazuri.
تلاش Luka 6:43
10
Luka 6:44
Watu huutambua mti kutokana na matunda yake. Ni wazi kwamba watu hawachumi tini katika michongoma, wala hawachumi zabibu katika mbigili.
تلاش Luka 6:44
صفحہ اول
بائبل
مطالعاتی منصوبہ
Videos