Luka 13:11-12
Luka 13:11-12 SCLDC10
Na hapo palikuwa na mwanamke mmoja aliyekuwa mgonjwa kwa miaka kumi na minane kutokana na pepo aliyekuwa amempagaa. Kwa sababu hiyo, mwili wake ulikuwa umepindika vibaya hata asiweze kusimama wima. Yesu alipomwona, alimwita, akamwambia, “Mama, umeponywa ugonjwa wako.”