Yohana 2
2
Harusi ya Kana
1 #
Yn 1:43
Na siku ya tatu palikuwa na harusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo. 2Yesu naye alikuwa amealikwa harusini pamoja na wanafunzi wake. 3Hata divai ilipowaishia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai. 4#Yn 19:26; Mt 12:48; Mk 1:24 Yesu akamwambia, Mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia. 5Mamaye akawaambia watumishi, Lolote atakalowaambia, fanyeni. 6#Mk 7:3,4 Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kunawa, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu. 7Yesu akawaambia, Jazeni mabalasi maji. Nao wakayajaza mpaka juu. 8Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa sherehe. Wakapeleka. 9Naye mkuu wa sherehe alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa sherehe alimwita bwana harusi, 10akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; na watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa. 11#Yn 1:14; 11:40 Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.
12 #
Mt 4:13; Yn 7:3 Baada ya hayo akashuka mpaka Kapernaumu, yeye na mama yake na ndugu zake na wanafunzi wake; wakakaa huko siku si nyingi.
Yesu atakasa hekalu
13 #
Kut 12:1-27
Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu. 14#Mt 21:12,13; Mk 11:15-17; Lk 19:45,46 Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng'ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi. 15Akasokota kikoto cha kamba, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng'ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao; 16#Lk 2:49 akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara. 17#Zab 69:9 Wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa imeandikwa, Wivu wa nyumba yako utanila. 18#Mt 21:23; Yn 3:2 Basi Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Ni ishara gani utuoneshayo, kwamba unafanya haya? 19#Mt 26:61; 27:40; Mk 14:58; 15:29 Yesu akajibu, akawaambia, Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha. 20Basi Wayahudi wakasema, Hekalu hili lilijengwa kwa muda wa miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu? 21#1 Kor 6:19 Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake. 22Basi alipofufuka katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa alisema hivi, wakaliamini lile andiko na lile neno alilolinena Yesu.
23Hata alipokuwapo Yerusalemu kwenye sikukuu wakati wa Pasaka, watu wengi waliamini jina lake, walipoziona ishara zake alizozifanya. 24Lakini Yesu hakujiaminisha kwao; kwa kuwa yeye aliwajua wote; 25#Mk 2:8 na kwa sababu hakuwa na haja ya mtu kushuhudia habari za mwanadamu; kwa maana yeye mwenyewe alijua yaliyomo ndani ya mwanadamu.
موجودہ انتخاب:
Yohana 2: RSUVDC
سرخی
شئیر
کاپی
کیا آپ جاہتے ہیں کہ آپ کی سرکیاں آپ کی devices پر محفوظ ہوں؟ Sign up or sign in
The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013.

: