1
Mathayo 27:46
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Ilipofika saa tisa, Isa akapaza sauti akalia, “Eloi, Eloi, lama sabakthani?” (maana yake, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”)
Compare
Explore Mathayo 27:46
2
Mathayo 27:51-52
Wakati huo huo pazia la Hekalu likachanika vipande viwili, kuanzia juu hadi chini. Dunia ikatetemeka na miamba ikapasuka. Makaburi yakafunguka na miili ya watakatifu waliokuwa wamekufa ikafufuliwa.
Explore Mathayo 27:51-52
3
Mathayo 27:50
Isa alipolia tena kwa sauti kuu, akaitoa roho yake.
Explore Mathayo 27:50
4
Mathayo 27:54
Basi yule jemadari na wale waliokuwa pamoja naye wakimlinda Isa walipoona lile tetemeko na yale yote yaliyokuwa yametukia, waliogopa sana, wakapaza sauti na kusema, “Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu!”
Explore Mathayo 27:54
5
Mathayo 27:45
Tangu saa sita hadi saa tisa giza liliifunika nchi yote.
Explore Mathayo 27:45
6
Mathayo 27:22-23
Pilato akawaambia, “Basi nifanye nini na huyu Isa aitwaye Al-Masihi?” Wakajibu wote, “Msulubishe!” Pilato akauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Lakini wao wakazidi kupiga kelele, wakisema, “Msulubishe!”
Explore Mathayo 27:22-23
Home
Bible
Plans
Videos