Waefeso Utangulizi
Utangulizi
Paulo aliandika waraka huu akiwa gerezani huko Rumi ili kuwatia moyo waumini wa jimbo la Asia. Waraka huu ulikuwa kama mwongozo uliokusudiwa kwa makundi kadhaa ya waumini wa Isa Al-Masihi. Zaidi ya hayo, kwenye waraka huu hakuna salamu za watu binafsi, wala hakuna matatizo maalum. Paulo alielezea kwamba jumuiya ya waumini ilianzishwa na Mwenyezi Mungu, akiwaelezea mpango wa Mungu wa tangu awali wa kuwaokoa watu wake kupitia Al-Masihi kwa imani. Mpango huu ulikuwako hata kabla ya ulimwengu kuumbwa. Mwenendo wa maisha mapya upo kinyume kabisa na ule wa maisha ya kale bila Al-Masihi.
Mwandishi
Mtume Paulo.
Kusudi
Kuwaimarisha waumini katika imani yao ya wafuasi wa Al-Masihi kwa kueleza asili na kusudi la jumuiya ya waumini wa Isa, ambayo ni mwili wa Isa Al-Masihi.
Mahali
Rumi.
Tarehe
Mnamo 60 B.K.
Wahusika Wakuu
Paulo, Tikiko, na waumini wa Efeso.
Wazo Kuu
Mpango wa Mwenyezi Mungu wa milele wa kuuokoa ulimwengu ulitimizwa kupitia kwa Al-Masihi katika mwili wake.
Mambo Muhimu
Umoja katika Al-Masihi na maisha mapya katika Al-Masihi (2:4-6), na umoja katika mwili wa Al-Masihi. Pia maisha wafuasi wa Al-Masihi wanayopaswa kuishi kuhusu ndoa, tabia, mwenendo, wazazi na watoto, watumishi na mabwana zao.
Yaliyomo
Mpango wa Mwenyezi Mungu, na wokovu wa wote wanaomwamini (1:1–2:22)
Siri ya Injili (3:1-21)
Maisha ya mfuasi wa Al-Masihi duniani (4:1–6:9)
Silaha za Mwenyezi Mungu, salamu za mwisho (6:10-24).
Currently Selected:
Waefeso Utangulizi: NENO
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.