Matendo 1:10-11
Matendo 1:10-11 NENO
Walipokuwa bado wakikaza macho yao kuelekea juu alipokuwa akienda zake mbinguni, ghafula, wanaume wawili waliovaa mavazi meupe wakasimama karibu nao. Wakasema, “Enyi watu wa Galilaya, mbona mnasimama mkitazama juu angani? Huyu Isa aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda mbinguni, atarudi tena jinsi hiyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.”