*Kutakuwa na vielekezo vya jua na vya mwezi na vya nyota. Huku nchini watu wa mataifa yote watapotelewa na mioyo wasipojua maana, mawimbi ya bahari yatakapokaza kuvuma na kutukutika. Ndipo, watu watakapozimia kwa woga na kwa kuyangoja mambo yatakayopajia pote, wanapokaa, kwani hata nguvu za mbingu zitatukutishwa. Hapo ndipo, watakapomwona Mwana wa mtu, anavyokuja katika wingi mwenye nguvu na utukufu mwingi.